Pages

Search This Blog

michuzi, MK,HAKI NGOWI, BONGO CELEBRITY, WATANZANIA, NGURUMO

Sunday 18 October 2009

wishing you Happy birthday and more to come abdallah

From Zefumo to Abdallah Shelufumo

On your birthday I wish you much pleasure and joy;
I hope all of your wishes come true.
May each hour and minute be filled with delight,
And your birthday be perfect for you!

Here's another year of experience






Pongezi kwa ngugu yetu Abdallah Shelufumo kwa kuzaliwa tena leo hii.

Blog yetu ya Zefumo ilikua pamoja bega kwa bega pamoja na mdau huyu ambaye vilevile ndio Mkurugenzi wa Blog hii ktk kufurahi siku ya kuzaliwa kwake.

Baadhi ys picha zilinazomuonesha Mdau mwenyewe hapo chini



Masanja anadai wahenga wanasema 'nchungaji mashuhuli kikwapa luwadudi" yaani

kazaliwa Abdallah Shelufumo kazaliwa Zefumoblogspot.

Picha zote na Zefumo.blogspot.com





Tuesday 13 October 2009

In those dayz


kipindi hicho shuja wetu wa tanzania na Afrika.



[JK.Nyerere.jpg]







Ila mazee tumetoka mbali, au unaniambiaje kilo.

zefumo iko pamoja na watanzania katika kuhitimisha maadhimishi ya kumbukumbu ya shujaa wa Afrika.
na Shelufumo



The memorial of Mwalimu Nyerere


Maisha ya Julius Nyerere

Sehemu ya Kwanza: Kuzaliwa na Malezi
Julius Kambarage Nyerere alizaliwa mwezi wa nne, tarehe kumi na mbili, mwaka elfu moja, mia tisa na ishirini na mbili katika nchi ya Tanganyika, na alikufa mwezi wa kumi, tarehe kumi na nne, mwaka elfu moja, mia tisa, tisini na tisa katika mji wa London. Alizaliwa mjini Butiama, karibu na pwani ya mashariki ya Ziwa la Victoria. Nyerere alikuwa mmoja wa watoto ishirini na sita wa babake, Nyerere Burito. Babake alikuwa kiongozi wa kabila la Zanaki na alikuwa na wake wawili. Pia babake alikuwa na fedha nyingi lakini hakuwa na elimu nyingi.
Wakati wa utoto wake, Julius Nyerere alichunga mifugo na alikuwa na maisha ya kawaida. Nyerere alikuwa mfuasi wa dini ya katoliki na watu waliomwona walisema alienda misa ya katoliki kila siku na hata wakati alikuwa mvulana, alifunga mara kwa mara. Kweli, mpaka alipokuwa na miaka kumi na mbili, Nyerere hakuwa na uzoefu na wazungu. Halafu aliingia shule huko mji wa Musoma, maili ishirini na sita kutoka nyumbani kwao (hili litaelezwa zaidi katika sehemu ya elimu yake.) Nyerere alibatizwa kuwa mkatoliki wakati alikuwa na miaka ishiniri. Nyerere alikua na kufika urefu wa futi tano na inchi sita na watu wote walisema alipenda sana kucheza na kufanya mizaha. Pia, wakati aliishi na kabila lake, alikata meno yake ya mbele na msumeno kuonyesha utamaduni wa kabila lake.
Maswali ya Ufahamu:

Habari na Abdallah Shelufumo, mmiliki wa Zefumo blogspot katika maadhimisho ya kumbukumbu za Baba wa Taifa, The World Hero Of Social Justice.



1. Nyerere alizaliwa nchi gani?
2. Nyerere aliishi miaka mingapi?
3. Nyerere alikuwa wa dini gani?

Sehemu ya Pili: Elimu
Julius Nyerere alienda Shule ya Msingi ya Serikali katika mji wa Musoma wakati alikuwa na miaka kumi na mbili. Alimaliza masomo ya miaka minne katika miaka mitatu kwa sababu alikuwa na akili sana, halafu alienda kusoma na Wavulana wa Shule ya Upili ya Serikali ya Tabora. Huko, alipata udhamini kwenda Chuo Kikuu cha Makerere. Ni muhimu kujua wakati alipata udhamini huo, Makerere kilikuwa chuo kikuu cha pekee katika Afrika ya Mashariki. Wakati alimaliza kusoma, alipata shahada.
Baada ya chuo kikuu, Nyerere alirudi Tanganyika na alifanya kazi katika Shule ya Upili ya St. Mary katika mji wa Tabora, katikati ya Tanganyika. Shule ya St. Mary ilikuwa shule ya kikatoliki. Huko, alifundisha masomo ya biolojia na
Kiingereza. Halafu, katika mwaka elfu moja, mia tisa na arobaini na tisa, alipata udhamini mwingine wa masomo. Wakati huu, aliweza kwenda chuo kikuu cha Edinburgh. Nilisoma vitu hivi katika wikipedia.com, na pia huko nilijifunza kwamba Nyerere alikuwa Mtanzania wa kwanza kusoma chuo kikuu cha nchi ya Wingereza na Mtanzania wa pili kupata digrii nje ya Afrika. Katika chuo kikuu cha Edinburgh, Nyerere alipata Shahada ya juu ya Sanaa katika Historia na Uchumi, mwaka elfu moja mia tisa, na hamsini na mbili. Katika Edinburgh, alisoma mkondo wa kufikiri unaoitwa “Fabian.” Mkondo wa “Fabian” wa kufikiri, ulijumuisha kundi la wataalamu wa Ujamaa wa Uingereza. Azimio la “Fabian” ni kuendeleza mawazo ya kijamaa kuongoa badala ya mapinduzi. Kwa hivyo, kwa sababu alijifundisha mawazo ya “Fabian,” alianza kufikiri mabadiliko mazuri sana yangepatikana ikiwa angeweza kuunganisha ujamaa na maisha ya Afrika. Wakati wa maisha yake, Nyerere aliitwa “mwalimu” kwa sababu ya kazi yake nyingi na elimu.
Maswali ya Ufahamu:
1. Kwa nini Nyerere alimaliza shule ya msingi mapema?
2. Nyerere alipata udhamini kwa nini?
3. Ni aina gani ya kufikiri aliyojifunza Nyerere huko chuo kikuu cha Edinburgh?

Sehemu ya Tatu: Ndoa na Familia
Wakati Julius Nyerere alikuwa mwalimu, na kabla ya maisha yake ya mwanasiasa, alioa mwanamke aliyeitwa Maria Magige. Maria alitoka kabila tofauti. Wanahistoria walisema alioa mwanamke wa kabila lingine kuonyesha dunia ilikuwa muhimu sana kusahau tofauti baina ya makabila na kusaidia umoja. Maria alimiliki duka dogo katika mtaa wa wenyeji wa Dar es Salaam. Pia, alikuwa rais wa Halmashauri ya Wanawake ya Tanganyika. Pamoja na Nyerere, alizaa watoto wanane, na leo watano wanaishi huko mjini Dar es Salaam.
Maswali ya Ufahamu:
1. Mke wa Nyerere alifanya kazi gani kabla ya kukutana na Nyerere?
2. Nyerere alikuwa na watoto wangapi?
3. Nyerere alifanya nini kujaribu kupata umoja baina ya makabila?

Sehemu ya Nne: Mchango Katika Jamii
Mchango mkuu wa Nyerere katika jamii ni kazi aliyofanyia serikali. Lakini kwanza nitaeleza kazi yake ya kufundisha. Nyerere alikuwa mwalimu wa historia, Kiingereza, na Kiswahili katika chuo cha St. Francis karibu na mji wa Dar es Salaam katika nchi ya Tanganyika. Huko, alianza shughuli ya siasa wakati alianza mradi wa TANU (Tanganyika African National Union) kupigania uhuru kwa nchi ya Tanganyika. Katika mwaka mmoja tu, TANU ilikuwa na watu wengi wapya na ilikuwa kiongozi wa miradi ya siasa katika Tanganyika. Kwa sababu Nyerere alianza kujihusisha na siasa, kwa ghafla alihitaji kuamua baina ya maisha ya mwalimu au maisha ya mwanasiasa. Watu wanasema Nyerere alisema “nilichagua kuwa mwalimu na ni ajali kwamba mimi ni mwanasiasa.” Alijiuzulu kutoka kufundisha, na Julius Nyerere alikuwa mwanasiasa kwa maisha yake.
Alisafiri ndani ya Tanganyika kusema na watu wengi na viongozi tofauti, kujaribu kupata msaada kwa harakati za uhuru wa Tanganyika. Katika mwaka elfu moja, mia tisa na hamsini na nne, alifaulu kuunganisha jamii mbalimbali kitaifa pamoja kusaidia harakati za uhuru. Nyerere alikuwa na ufarisi wa kusema uliomsaidia wakati alisema na UN (Umoja wa Mataifa) kuhusu uhuru wa Tanganyika. Katika mwaka elfu moja, mia tisa na hamsini na nane, aljiunga na Colonial Legislative na alishinda uchaguzi wa Waziri Mkuu katika mwaka elfu moja, mia tisa na sitini.
Nyerere alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Tanganyika mwezi wa kumi na mbili, tarehe tisa, mwaka elfu moja, mia tisa na sitini na moja, mwaka wa kwanza wa kujitawala kwa Tanganyika. Mwaka mmoja ulipita na Nyerere alishinda uchaguzi kuwa rais wa Tanganyika katika mwaka elfu moja, mia tisa, sitini na mbili, mwaka wa uhuru wa Tanganyika, jamhuri mpya. Pia, ni muhimu kujua kwamba Nyerere alifaulu kuunganisha kisiwa cha Zanzibar na Tanganyika bara pamoja kuunda nchi ya Tanzania katika mwaka elfu moja, mia tisa, sitini na nne, baada ya mapigano huko Zanzibar yaliyomaliza utawala wa Jamshid bin Abdullah, kiongozi wa Zanzibar.
Julius Nyerere aliendelea kuwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania mpaka mwaka elfu moja, mia tisa, na themanini na tano. Wakati alikuwa rais, Nyerere alikuwa na matatizo mengi kwa sababu mwaka elfu moja, mia tisa na sitini, Tanzania ilikuwa nchi maskini sana kulinganisha na nchi zingine za dunia. Tanzania ilikuwa na deni kubwa sana na vitu viliongezeka bei. Kusaidia nchi yake, Nyerere aliamua kujaribu ujamaa na maisha ya pamoja vijijini, na utaifishaji. Aliandika dhana zake katika Azimio la Arusha la Mwaka elfu moja, mia tisa, sitini na saba, lililosema kuhusu maendeleo ya mashamba. Watu walihimizwa kuishi na kufanya kazi pamoja katika vijiji vilivyokusudiwa kusambaza desturi ya utamaduni wa Tanzania na kuunda umoja. Watu wanafikiri Nyerere alishinda matatizo mengi ya Tanzania na aliunda jamii ya umoja huko.
Baada ya shughuli ya Rais, Nyerere aliendelea kusaidia jamii yake. Alikuwa mwenyekiti wa Kundi: Chama cha Mapinduzi (CCM). Baada ya miaka michache, aliacha shughuli yake ya mwanasiasa kwa sababu alikuwa mzee. Alipumzika katika shamba lake huko Butiama, mjini alipozaliwa. Katika mwaka elfu moja, mia tisa na tisini, aliacha kuwa mwenyekiti wa CCM lakini aliendelea kufanya kazi ya haki za kibinadamu. Kwa mfano, katika mwaka elfu moja, mia tisa na tisini na sita, alikuwa mwamuzi mkuu wakati wa ugomvi katika nchi ya Burundi. Kwa bahati mbaya, alipata ugonjwa wa kansa ya leukemia, na alikufa mjini London mwezi wa kumi, tarehe kumi na nne, mwaka elfu moja, mia tisa, tisini na tisa.
Maswali ya Ufahamu:
1. Nyerere alikuwa rais wa Tanzania kati ya miaka gani?
2. Ni kisiwa kipi Nyerere aliunganisha na Tanganyika kuwa Tanzania?
3. Baada ya kazi ya rais, Nyerere alifanya nini?

Sehemu ya Tano: Maoni Yangu Kumhusu
Kwanza, ningesema Julius Nyerere alikuwa mtu wa athari kubwa sana. Kupitia wajibu wake wa kutetea haki za kibinadamu katika nchi yake ya Tanzania na katika dunia yote, alielimisha watu wengi. Julius Nyerere alifanya kazi tofauti: alikuwa mwalimu na mwanasiasa, lakini katika kazi zote, alijaribu kufanya jamii bora. Nyerere alikuwa mwanasiasa wa kanuni na akili sana. Alitumia ubongo wake kusaidia watu wa Tanzania kuishi maisha bora. Pia, alikuwa mwaminifu, kwa sababu wakati alikuwa rais alitumia msaada wote kusaidia Tanzania. Nyerere alikuwa na elimu nyingi, na kwa hivyo aliweza kusema waziwazi na kuandika katiba muhimu. Utafiti wangu uliniambia kuwa Nyerere alikuwa tayari kila siku kufanya kazi na vyama tofauti sana, na alisikia maoni ya watu wote. Tunaweza kuona alifanya kazi na Uingereza kusaidia watu wake. Pia, alikuwa sababu kubwa sana ya Tanzania kupata uhuru.
Maswali ya Ufahamu:
1. Kazi mbili tofauti za Nyerere zilikuwa nini?
2. Nilisema nini kuhusu kazi tofauti ya Nyerere?
3. Kwa sababu Nyerere alipata elimu nyingi, aliweza kufanya nini?

Sehemu ya Mwisho: Maswali ya Mjadala
1. Unafikiri kuwa mmoja wa watoto ishirini na sita kuliathirije Nyerere?
2. Kwa maoni yako, nini ni mchango mkubwa wa Nyerere katika jamii?
3. Unakubalina na dhana za Nyerere kuhusu Ujamaa?
4. Unafikiri nini katika maisha ya Nyerere kilimfanya kutaka kusaidia dunia?
5. Kwa nini Nyerere aliweza kuipata Zanzibar?
6. Unafikiri dini ya Katoliki ilimsaidia Nyerere?
7. Kwa maoni yako, elimu ni muhimu kwa nini?
8. Kwa nini Nyerere hakuona wazungu mpaka alipokuwa na miaka kumi na mbili?
9. Kwa nini Nyerere alikufa? Leo, kuna tiba kwa ugonjwa wake?
10. Je, unakubalina na maoni yangu kumhusu?

Marejeleo

“Julius Nyerere.” Wikipedia: The Free Encyclopedia. 10 May 2007. Wikimedia Foundation, Inc. 12 May 2007. .
Robbins, James. “Julius Nyerere: The conscience of Africa.” 14 October 1999. BBC World: Africa. 12 May 2007. .
Smith, Mark. “Julius Nyerere, Lifelong Learning and Informal Education.” 20 May 2007. Infed. 23 May 2007. .
Simmons, Charles E. “President Julius Nyerere: A Great Teacher and Devoted African Leader.” 12 May 2007. .

No related posts.











Thursday 8 October 2009

dreamz for AC Millan


Ramadhani mwanga a.k.a kipaji[Yahiiiiiiii......., povu] kupatikana kama Nyota wa msimu katika ligi chini ya miaka 21 ikifahamika kama serengeti boyz bila shakawatanzania wananisoma huko nchini Italy.
Nyota huyo mwenye uwezo wahali ya juu ambae ni raia wa Tanzania, alikua na ndoto kubwa katika fani ya mpira, ambapo alipokua secondary alishatunukiwa tuzo ya uchezaji bora katika shule ya Mtakatifu matayo huko tanzania.
juhudi zake zilimfanya akachukuliwa na Chelsea FC nchini Uingereza katika timi ya chini ya miaka 18, kama picha zinavyoonesha hapa chini akiwa stanford bridge.



hatahivyo nyota huyo hakudumu kwa muda mrefu stanford bridge kwa sababu ya kimaslahi kwani aliamini kwa kiwango chake na pesa mambayo alikua akilipwa si sahii, na hivyo kuhama jiji la London na kuelekea nchini Italy ambapo Jose Mourinho alimuahidi dau nono ambapo nyota huyo basi ndipo anaporock kwa sasa, kama picha zinavyoonesha akila tizi





picha na Zefumo.

heppi bethday G


Hatimaye Globilly britho a.k.a the big G bila shaka uncle nahiii {mr. nice} ananisoma kuzaliwa tena baada ya masaa 48 kuanzia sasa[10 oct].
blog yetu ya Zefumo yenye makao yake makuu Reading jijini London, ilifanikiwa kufanya mahojiano ya uso kwa uso na muhusika{glory] juu ya tafrija hiyo inayo tarajiwa kufanyika tarehe 10 oct kuanzia majira ya saa 12 jioni mpaka kuchwee ndani ya 22 Old Kennels Court Rg30 3ns.

kwa niaba ya mhusika Zefumo imepewa nafasi ya kuwakaribisha ndugu, jamaa na marafiki wote
wanaohusika.
kutakuwepo na itifaki ya kufa na mtu muziki mkubwa, vyakula vya kusaza, vinywaji mbalimbali bila kusahau maji yetu ya uzima, bila shaka uncle na nihii[ching'oro] ananisoma.
Hatahivyo Zefumo ilijaribu kumtafuta jamaa mwenyewe Levin Boaz a.k.a Mr. nice kwa taarifa zaidi lakini hakuweza kupatikana.

kwa niaba ya Mh. Abdallah Shelufumo Zefumo kwa maranyingine tena inatoa pongezi kwa dada yetu Glory kwa kutimiza miaka 2__ ?
Mungu akubaruki


picha na Abdallah Shelufumo.