Pages

Search This Blog

michuzi, MK,HAKI NGOWI, BONGO CELEBRITY, WATANZANIA, NGURUMO

Tuesday 8 March 2011

MABOMU GONGO LA MBOTO

Zefumo, Je kweli hii ni haki. ??

WANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’ na Mrisho Mpoto ‘Mjomba’, Jumapili iliyopita walijikuta wakimalizia siku kwenye Kituo cha Polisi cha Sitakishari, Ukonga, jijini Dar es Salaam kwa madai makuu mawili. 

Wasanii hao walishikiliwa Februari 20, 2011 kwa madai mosi, kumtusi mwanajeshi mmoja wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ‘JWTZ’ (jina halikupatikana), pili kurekodi video ya wimbo wao mpya wa Gongo la Mboto kwenye eneo la maafa bila kibali.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha uhakika, mastaa hao ‘walidakwa’ Jumapili saa 9:00 alasiri na kuwekwa katika Kituo cha Polisi cha Msimbazi, Kariakoo, Dar na baadaye kupelekwa Sitakishari ambako ndiko kwenye malalamiko yao.


Ilidaiwa kuwa, kisa kilianzia Februari 19, 2011 alasiri ambapo wawili hao walikuwa wakirekodi video ya wimbo huo maeneo ya maafa, Gongo la Mboto.

Chanzo kikasema, walifika eneo ambalo bado kulikuwa na bomu nje ya nyumba moja, wakaendelea kurekodi.
“Mara, akatokea mtu na kujitambulisha kwao yeye ni mwanajeshi,” kilisema chanzo hicho.

Kikaendelea: “Akawauliza kama wana kibali cha kuwaruhusu kurekodi video eneo hilo, wao wakajitetea kwa kujibu ni wasanii wanachukua picha kwa ajili ya muziki ambapo lengo ni kuwapa pole waathirika wa milipuko ya mabomu.”

Chanzo kikaendelea kusema kuwa, wananchi waliokuwa wakishuhudia uchukuaji huo wa picha walianza kumsemea mbovu ‘mjeshi’ huyo wakimtaka awaache wasanii hao wafanye kazi yao.

“Kitendo cha kusakamwa na wananchi kilimkera yule mwanajeshi, kwa hasira  akalichukua bomu lililokuwa chini, akaliweka begani na kuondoka nalo,” kilisema chanzo.

Jumapili, saa tano, Mpoto alipokea simu ikimtaka yeye na Diamond kufika Kituo cha Polisi Msimbazi.

Ndani ya kituo hicho, habari zinadai, walijulishwa makosa yao kwamba, walimtukana mwanajeshi huyo na pia walikuwa wakirekodi picha za maafa kwa ajili ya muziki ambazo zingeichonganisha serikali na wananchi lakini wakatakiwa kupelekwa Sitakishari kwa maelezo zaidi.

Jumatatu asubuhi, Risasi Mchanganyiko lilimpigia simu Diamond na kumuuliza kuhusu mkasa huo ambapo alikiri kutokea.

Akasema: “Tulidakwa jana saa tisa pale Msimbazi, baadaye tukapelekwa Sitakishari.”

Akaongeza: “Unajua yule mwanajeshi alidai tumemtukana. Halafu eti picha tulizokuwa tunarekodi zinaweza kuwafanya wananchi wakaichukia serikali yao.”

Akaendelea: “Mkuu wa Kituo cha Sitakishari alituhoji, kisha akataka video, akaziangalia, akaturuhusu kuondoka saa mbili. Lakini alisema leo (Jumatatu) atatuita tena.



Kwa upande wake, Mjomba Mpoto naye alikiri kukamatwa na polisi huku akisema bado maafande hao wanazishikilia kanda zenye video hizo ili wazichunguze kama zina uchochezi ndani yake.

“Ni kweli yametukuta na hivi ninavyokwambia kaseti zetu zipo polisi, eti wanadai mpaka wazichunguze lakini kuhusu wimbo, utaendelea kupigwa redioni kama kawaida,” alisema Mpoto.

Risasi Mchanganyiko liliongea na afande mmoja wa Kituo cha Polisi cha Sitakishari ambapo alisema yupo nje ya ofisi lakini hakutaka kukiri wala kukataa kushikiliwa kwa wasanii hao kwa madai si msemaji wa jeshi hilo.

Kwa upande mwingine, Mpoto alipokuwa akizungumza kwenye Kipindi cha Jahazi cha Clouds FM juzi alisema, polisi waliwarudishia mkanda wa video waliokuwa wakirekodi baada ya kutoa baadhi ya vipande ambavyo hawakupenda vitumike.
Na Abdallah Shelufumo