Pages

Search This Blog

michuzi, MK,HAKI NGOWI, BONGO CELEBRITY, WATANZANIA, NGURUMO

Monday 28 September 2009

blog yenu ya ze fumo ambayo ndio blog ya kwanza kwenye sayari
kuchapisha picha za Meddy akiwa ÔbenetiÕ na mkewe, Zaitun Kessy Mpakanjia ambazo zilipigwa muda mfupi baada ya wawili hao kufunga pingu za maisha.Picha hizo ambazo gazeti hili limezinasa kupitia kwa vyanzo vyake, zilipigwa kwa njia ya simu wakati Meddy na Zaitun walipokuwa wameketi kitandani kwenye moja ya vyumba vya nyumbani kwa bibi harusi huyo.Katika picha hizo, marehemu Meddy licha ya kwamba yupo jirani na mkewe na alikuwa ametoka kwenye shughuli ya kufunga ndoa ambayo ni tendo la furaha lakini yeye anaonekana hana raha na amepooza.Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, hali ya Kitendawili ilianza kubadilika wakati akiwa anafunga ndoa na ilifikia kipindi alijieleza wazi wazi kwamba alikuwa akijisikia vibaya.Vyanzo vyetu vinaeleza kuwa, kutokana na hali ya Kitendawili kubadilika na kujieleza kuwa hajisikii vizuri, ilibidi maswali kwenda kwa bwana harusi ambayo kimsingi yalitakiwa kujibiwa na Meddy, siku hiyo yajibiwe na kaka yake, Abdul Mpakanjia.ÒBinadamu ni vipofu kwenye suala la kifo, lakini pale pale harusini alilalamika anaumwa na ndiyo maana maswali ya bwana harusi aliyajibu kaka yake, Meddy hakujibu,Ó alisema mtoa habari wetu na kuongeza:ÒMimi nmachukulia kuwa umauti ulianza kumzunguka tangu wakati akiwa kwenye ndoa, kwa sababu muda mfupi baada ya kufika nyumbani alilalamika tumbo linamuuma sana, siku hiyo alilala kwa tabu, kesho yake alipopelekwa hospitali alifariki dunia.Meddy, alifariki dunia Jumatatu ya wiki hii kwenye Hospitali Kuu ya Jeshi, Lugalo, Dar es Salaam na kuzikwa siku iliyofuata (Jumanne) kwenye makaburi ya Kisutu, jijini Dar.Marehemu ameacha mjane, Zaitun na watoto wanne, Abdulrahim, Ibrahim, Karim na Abdulrahman a.k.a Rahmanino ambaye alizaa na aliyekuwa mkewe, Mbunge wa Viti Maalum, UVCCM, Amina Chifupa Maboga.




na abdallah shelufumo

No comments:

Post a Comment