Pages

Search This Blog

michuzi, MK,HAKI NGOWI, BONGO CELEBRITY, WATANZANIA, NGURUMO

Monday 28 September 2009

burihani mpakanjia

Zaitun ambaye anaonekana ukurasa wa mbele wa gazeti hili, alifunga ndoa na Meddy Jumapili iliyopita na kuishi naye kwa saa kumi na saba kabla ya kifo cha mumewe. Hata hivyo, gazeti hili lina mengi ambayo yameibuka kufuatia kifo hicho kilichotokea ghafla, moja ya hayo ni kugundulika kuwa, marehemu alishaandika mirathi ya nyumba zake mbili, zilizoko Sinza na Mbezi, jijini Dar es Salaam. Habari zinasema kuwa, marehemu alimwandika mtoto wake wa mwisho, Abdulrahman Mohamed Mpakanjia a.k.a Rahmanino kurithi ule mjengo wa pale Sinza-Mori. Mbali na huyo, mtoto mwingine ambaye amepata nyumba kupitia mirathi hiyo ni Rahim Mohamed Mpakanjia ambaye anakuwa mmiliki wa nyumba ya Mbezi. Watoto wengine wa marehemu, Ibrahim na Karim Mohamed Mpakanjia, wote wamerithi nyumba mbili zilizopo, Tandika, wilayani Temeke, Dar kwa kila mmoja kuchukua ya kwake. Kauli ya marehemu aliyoiacha kwa mkewe mpya, Zaitun wakati akipelekwa Hospitali Kuu ya Jeshi, Lugalo ni jambo lingine nyuma ya msiba huo. Habari zinasema, marehemu Mpakanjia alimwambia mkewe huyo kwamba, anapelekwa hospitali, lakini hatopona na hivyo ana uhakika kuwa, anamwacha katika eda. Zaitun alilithibitishia gazeti hili kuwa, kweli marehemu alitamka maneno hayo, licha ya kwamba awali hakuwa amejua alilenga nini. “Marehemu wakati anapelekwa hospitali aliniambia, mke wangu nakuhurumia, napelekwa hospitali lakini nakuacha eda,” alisema Zaitun. Aidha, mapya mengine ambayo yaliutikisa msiba wa Meddy ni ndogo ndogo ambazo zimelifikia gazeti hili kwamba baadhi ya ndugu wa marehemu wanamnyanyapaa Zaitun kwa maelezo kuwa yeye si mke halali. Ushakunaku wetu msibani umebaini kuwa mpaka juzi, Zaitun alikuwa hajavalishwa mavazi rasmi ya mwanamke mjane ambayo huvaliwa wakati wa eda. Katika hilo, Amani limebaini kwamba kulikuwa na mikakati ya chini kwa chini kutoka kwa baadhi ya ndugu wa marehemu, waliotaka ‘kutaifisha’ haki zote za mjane huyo.

get informed by ze fumo

No comments:

Post a Comment